RIHANNA SASA AAMUA KUMUANIKA "KIBOKO YAKE"

BAADA ya kuendesha penzi la kujifichaficha kwa muda mrefu sasa, mrembo Rihanna ameamua kuweka mambo hadharani baada ya kunaswa akiponda raha na mpenzi wake, Hassan Jameel raia wa Saudi Arabia.

Raia huyo wa Arabia ambaye familia yake ina utajiri wa dola bil 1.5 alinaswa na Rihanna wakiponda raha katika jiji la Boston.

Wawili hao walikutwa kwenye mgahawa wa Dante wakipata chakula cha mchana pamoja huku wakitaniana na kupigana mabusu hadharani.


Kabla ya hapo wawili hao walipigwa picha wakiwa wanakunywa kahawa kwenye fukwe za Ibiza nchini Hispania na muda mfupi baadaye walionekana katika jiji la London.

No comments