RIYAD MAHREZ ANUKIA FC BARCELONA

WINGA wa timu ya Leicester City, Riyad Mahrez mwenye miaka 26 anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya kuwepo ofa ya kujiunga na timu ya Roma na Barcelona.

Staa huyo wa Algeria ameweka ofa isiyopungua mil 50 na Barcelona ili aweze kujiunga nayo mwishoni mwa msimu.


Barcelona wana nafasi kubwa ya kumsajili baada ya kuonyesha nia ya kumnasa muda mrefu tangu wakati wa dirisha kubwa la usajili lililopita.

No comments