RONALDO AKATAA MKATABA MPYA REAL MADRID ...ataka kutimka mwishoni mwa msimu


Cristiano Ronaldo ameripotiwa kukataa mkataba mpya Real Madrid na anataka klabu hiyo impige bei mwishoni mwa msimu huu.

Ronaldo ambaye mara kadhaa alishaweka wazi kuwa hataki kurefusha mkataba wake wa sasa unaoisha mwaka 2021, iliaminika kuwa alitaka kuondoka Real Madrid kiangazi kilichopita.

Mwanahabari wa Kihispania, Edu Aguirre anayekitumikia kituo cha El Chiringuito, amedai Ronaldo amemwambia rais wa Real Madrid Florentino Perez juu ya uamuzi wake wa kutaka kutimka.No comments