ROONEY ‘AFUFUKA’ APIGA ‘HAT-TRICK’ EVERTON IKIIANGAMIZA WEST HAM 4-0 ...Chelsea nayo mwendo mdundo


Wayne Rooney  amedhihirisha kuwa bado ni mshambuliaji hatari baada ya kuifunga West Ham mabao matatu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ambao Everton waliibuka wababe kwa ushindi wa 4-0.

Rooney akaongoza maangamizi dhidi ya kocha wake zamani David Moyes kwa kufunga katika dakika ya 18, 28 na 66 huku beki Ashley Williams akifunga goli la nne dakika ya 78

Katika mchezo mwingine wa Premier League uliochezwa Alhamisi usiku, Chelsea ikaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Swansea City kwa bao lililofungwa na beki Antonio Ruediger kunako dakika ya 55.

Matokeo yote ya Ligi Kuu ya England ya mechi za Alhamisi ni:
AFC Bournemouth 1 - 2 Burnley
Arsenal 5 - 0 Huddersfield Town
Chelsea 1 - 0 Swansea City
Everton 4 - 0 West Ham United
Manchester City 2 - 1 Southampton
Stoke City 0 - 3 Liverpool

No comments