SAAD ALLY "MACHINE" AREJEA MSONDO NGOMA AKISEMA: "MTOTO KARUDI KWA MAMA"

MCHARAZAJI mahiri wa ngoma ndogo “Drums”, Saad Ally  “Machine” amejifananisha na mtoto aliyerudi kwa mama yake baada ya hivi karibuni kurejea upya kuitumikia bendi yake ya zamani, Msondo Ngoma Music Band.

Kwa muda mrefu sasa Saad alikuwa amehamishia mabegi ndani ya Talent Band ambayo iko chini ya mwimbaji mkongwe wa miondoko ya dansi Bongo, Hussein Jumbe “Mzee wa Dodo” ambapo takriban wiki mbili nyuma ameanza kuonekana tena Msondo Ngoma.


Akipiga stori na Saluti5, Saad amesema kuwa: “Hii ni bendi yangu ya nyumbani na watu wasinishangae nikiondoka na kurudi baada ya muda, ni sawa na mtoto amerudi kwa mama yake tu.”

No comments