SENTESI TATU ZA JOSE MOURINHO JUU YA KUREJEA KWA POGBA


Paul Pogba amerejea Manchester United kwa kishindo baada ya kufunga bao moja na kutengeneza moja katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Newcastle.

Kocha wake Jose Mourinho akammiminia sifa kibao kiungo huyo aliyekuwa akiiuguza maumivu ya nyama za paja kwa kusema:

"Pogba ni wa daraja jingine. Hivi ndivyo tulivyokuwa mwanzoni mwa msimu tukiwa na Paul na Nemanja  Matic, wakiwa wanaimarika kwa pamoja na wanakuwa kama ndio injini ya timu," Mreno huyo aliiambia BT Sport.

"Tulikuwa tukishindwa katika mapambano kutokana na kwamba timu nyingine zilikuwa na wachezaji wazuri na walikuwa na viwango tofauti.   

“Nililiacha mikononi mwa Paul kuamua ni muda gani atacheza. Tulifanya uamuzi sahihi kumpumzisha katika muda mwafaka kwa kweli ameonyesha kiwango kikubwa.”   

No comments