SERGIO AGUERO YUKO FITI KUIVAA LEICESTER JUMAMOSI HII


Sergio Aguero amejithibitishia  yeye mwenyewe kuwa yuko fiti kuitumikia Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Leicester Jumamosi hii.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina aliaunguka na kupoteza fahamu katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya nchi yake na Nigeria.
Lakini amewaondoa mashaka mashabiki wa Manchester City baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba yuko fiti.

"Niko tayari kwa mechi ya Jumamosi. Twendekazi Man City!", aliandika Aguero.

No comments