SHABIKI WA MSONDO NGOMA MOROGORO ASEMA "KILA WIKI NATUA DAR KWA AJILI YA BABA YA MUZIKI"

MARINGO “mzee wa Morogoro” ni kati ya mashabiki wa muziki wa dansi aliyekiri kuwa pamoja na mvua kubwa iliyokung’uta Jumamosi hii, lakini alilazimika kutoka Mji Kasoro Bahari hadi jijini Dar es Salaam kufuata burudani ya Msondo Ngoma.

Akiongea na Saluti5, mzee wa Morogoro amesema kwamba amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara kutokana na mapenzi aliyonayo kwa bendi hiyo inayokusanya wanamuziki wengi wenye uwezo mkubwa jukwaani.


“Mara nyingi huwa nakuja Dar es Salaam kila wikiendi ninapopata nafasi ili kuburudika na Msondo Ngoma na kama ulivyoona, ninapofika lazima niingie kati kucheza sambamba na wana Msondo Family,” amesema shabiki huyo.

No comments