SHAKIRA: TATIZO LA KOO LILIKATISHA ZIARA YANGU UJERUMANI

MREMBO Shakira amesema kuwa kukatisha kwake ziara ya muziki nchini Ujerumani kulitokana na tatizo la koo ambalo alikumbana nalo siku chache kabla ya tamasha hivyo akalazimika kupumzika kwa muda.

Ziara hiyo ya “El Dorado” ilikuwa ifanyike mwezi huu lakini imeghailishwa mpaka Januari mwakani ilikupisha matibabu yake.

“Ninapaswa kuangalia kwanza afya yangu kwasababu nimepitia wakati mgumu hivyo ratiba ya mwezi huu haitawezekana mpaka januari mwakani,” alisema Shakira.

“Inaumiza kwasababu nilijiandaa mwezi mzima lakini imeshindikana baada ya kuambiwa na daktari kuwa napaswa kupumzika kwanza,” aliongeza.


Mrembo huyo ameolewa na beki wa Barcelona, Gerrald Pique ambaye walikutana nae katika fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

No comments