SIKU ZA PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG ZINAHESABIKA BORUSSIA DORTMUND …Liverpool, Chelsea zishindwe zenyewe


Hakuna ubishi kuwa siku za Pierre-Emerick Aubameyang zinahesabika Borussia Dortmund baada kufanya 'utoto' ulioinyima timu yake ushindi dhidi ya Schake 04.

Katika mchezo huo wa  Bundesliga uliochezwa siku ya Ijumaa, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Garbon, aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 12, lakini dakika ya 72 akatolewa kwa kadi nyekundu huku Borussia Dortmund ikiwa mbele kwa bao 4-2.

Schake 04 wakautumia vizuri upungufu wa Dortmund na kufanya mwisho wa mchezo matokeo yasomeke 4-4.

Baada ya mchezo huo, kocha wake   na wachezaji wenzake wakaonyesha hasira za wazi juu ya utovu wake wa nidhamu na kwa mujibu wa gazeti la Bild la Ujerumani ni kwamba siku za Aubameyang klabuni hapo zinahesabika.

Kipa Roman Weidenfeller akasema mshambuliaji huyo amefanya jambo la kijinga huku  kocha  Peter Bosz akisema Aubameyang aliharibu kila kitu. 

Chelsea na Liverpool ni vilabu viwili vinavyohusishwa sana na usali wa wa Pierre-Emerick Aubameyang.

No comments