SIMBA, YANGA SASA RUKSA UWANJA WA TAIFA

SERIKALI kupitia kwa waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe imeruhusu kutimika kwa uwanja wa Taifa uliokuwa unafanyiwa ukarabati.

Sasa uwanja huo utaanza kutimika rasmi Novemba 24 mwaka huu kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania bara.

Dkt. Mwakyembe ameishukuru kampuni ya sportPesa ambayo ndio imebeba jukumu la kukarabati uwanja huo.

“Nashukuru kuona nyasi za uwanjani zimeota vizuri na unapendeza, kikubwa nashukuru kwa vijana wetu sita ambao wamefundishwa namna ya kutunza viwanja,” amesema Dkt. Mwakyembe.

Mkuu wa Oparesheni SportPesa, Luca Neghesti amethibitisha ukarabati wa uwanja utakamilika Novemba 21 na utadhibitiwa Novemba 24 mwaka huu ukiwa tayari kwa matumizi.

“Kazi ya kukarabati sehemu ya kuchezea imekamilika na nyasi zilizooteshwa zimeota vizuri na zimeshika hivyo upo tayari kutumika,” alisema Luca.


Klabub ya Simba na Yanga ambavyo huutumia uwanja wa taifa kwa mechi zao za nyumbani huenda zikarejea kwenye uwanja huo kuanzia Novemba 24 baada ya kukabidhiwa kwa serikali.

No comments