SINZA SOUND BAND YAAHIDI MAMBO MAZITO ZAIDI LION HOTEL WIKI HII

SINZA Sound Band chini ya Said Kaunga imeendelea kufanya mambo makubwa ya kiburudani ndani ya Lion Hotel, Sinza jijini Dar es Salaam na kujikuta ikizidi kuvuta hisia za mashabiki wa muziki wa dansi.

Bendi hiyo inayotumbuiza ukumbini hapo kila wiki katika siku za Ijumaa na Jumamosi, imeonekana kumudu kikamilifu kukuna na kukwangua nyoyo za mashabiki kiasi cha kuzidi kumiminika kila uchao.

Wiki hii kama kawaida yao, Sinza Sound Band wataungurumisha mangoma ndani ya kiwanja hicho Ijumaa na Jumamosi ambapo mitindo mbalimbali ya muziki kutoka kote ulimwenguni itaporomoshwa.

Bosi said Kaunga ameiambia Saluti5 kuwa kikosi chake kimejipanga kikamilifu kuhakikisha kila shabiki atakayefika kuburudika ataondoka nyumbani akiwa ameridhika na nafsi yake baada ya muziki kumalizika.

“Kila kitu kiko poa na kwamba tumezidi kuongeza ladha ambazo tuna imani zitachochea kuwafanya wapenzi wetu kuifurahia zaidi bendi yao hii,” amesema Kaunga ambaye ni kati ya waimbaji wenye sauti za kumtoa nyoka pangoni.

No comments