Habari

SIO KWA KICHAMBO HIKI CHA MOURINHO KWENDA KWA ANTONIO CONTE!!

on

Kuelekea mechi ya Premier League kati ya Chelsea na Manchester United ndani ya dimba la Stamford Bridge, Jose Mourinho amempiga kijembe Antonio Conte na kumtaka aache kulia juu ya wachezaji majeruhi.
Chelsea imekuwa ikiyumba bila kiungo N’Golo Kante huku Victor Moses na Alvaro Morata wakisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, hatua ambayo imekuwa ikitajwa na kocha Antonio Conte kama sababu ya kususua kwa timu yake katika baadhi ya mechi.
Lakini Mourinho anakataa kabisa kisingizio hicho na kusema kama ni suala la majeruhi, basi yeye angekuwa akilia kila kila wiki.
Manchester United imemkosa Paul Pogba kwa mechi 11, Marcos Rojo bado ni majeruhi tangu mwishoni mwa msimu uliopita, Marouane Fellaini naye yuko nje ya dimba achilia mbali wachezaji  wake kadhaa ambao wamekuwa wakiumia akiwemo beki tegemeo Eric Bailly.
“Najua kuwa nimekuwa mlalamishi kwa baadhi ya mambo lakini kamwe sijawahi ‘kuomboleza’ kwaajili ya majeruhi, pengine ningepaswa kulia kila wiki,” anaeleza Mourinho.
“Naamini kocha mwingine yeyote angekuwa akilia kila siku ‘Oh sina Pogba, oh mechi zote kubwa kama za Liverpool, Chelsea, Spurs bila Pogba, mechi za Champions League bila Pogba’. Mimi sizungumzi kuhusu Pogba hata mara moja, labda pale tu ninapoolizwa kuhusu maendeleo yake”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *