THABIT ABDUL ASEMA: ‘TAABAB HAIJAFA LABDA DANSI NDIO NDIO IMEKUFA’


Mpapasa kinanda, mtunzi na mkurugenzi wa kundi la Wakali Wao Modern Taradance, Thabit Abdul amesema taarab haijafa, labba muziki wa dansi ndio umekufa.

Thabit Abdul ameyasema hayo mchana huu wakati akihojiwa na kipindi cha Tam Tam za Mwambao cha kituo cha East Africa Radio kinachoongozwa na Mwanne Othman.

“Hii kauli naipinga kila siku, haiwezekani kulinganisha taarab na dansi kwa sasa hivi wakati karibu bendi zote za dansi zinapiga kiingilio kinywaji,” alisema Thabit ambaye ana uwezo wa kupiga karibu ala zote za muziki wa dansi na taarab.

“Ukiangalia bendi kubwa za taarab kama Wakali Wao, Mashauzi, Jahazi, Yah TMK na Ogopa Kopa zinapiga kwa kiingilio, lakini katika bendi za dansi ni Bella peke yake ndio anapiga kwa kiingilio, bendi zingine zote zilizobakia zina show kibao za bure (kiingilio kinywaji). Sasa hapo ipi imekufa kati ya taarab na dansi?” aliongeza Thabit Abdul.

No comments