‘TIBA’ YA ROMELU LUKAKU NI PAUL POGBA TU, HAKUNA NAMNA NYINGINE


KIUNGO nyota wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes, amesema kukosekana kwa Paulo Pogba na kutokuwa kwenye kiwango kwa Henrikh Mkhitaryan, ndiyo sababu ya ukame wa mabao kwa Romelu Lukaku.

Lukaku amecheza michezo sita bila kutikisa nyavu baada ya kuanza kibarua kwa kasi United akipachika mabao 11 katika michezo 10.

Akizungumza na BT Sport, Scholes alisema: "Nadhani kama Pogba atarudi, atafanya vitu tofauti kwa jinsi wanavyocheza.
"Lukaku anahitaji kujifanyia mengi, lakini Pogba atafanya tofauti. (United) Wanakosa mchezaji wa kuiunganisha timu pamoja."

Pogba aliyekosa michezo 11 iliyopita akiuguza maumivu ya nyama za paja, amerejea Carrington, lakini anaonekana kuwa hatakuwa tayari kwa safari ya Stamford Bridge kuivaa Chelsea siku ya Jumapili.

No comments