TOTOO ZE BINGWA ASEMA: ‘SIJAJA KUIMBA, NIMEKUJA KUCHEZESHA’ … aondoka kwa Bella na kuamua kujitegemea


Rapa maarufu wa Malaika Band, Totoo Ze Bingwa ameamua kuwa msanii wa kujitegemea na tayari ana nyimbo moja mkononi.

Bendi ya mwisho Totoo kuitumikia ni Malaika Band chini ya Christian Bella, lakini sasa anasimama kama msanii anayejitegemea, akitandika show zake binafsi kwa mfumo wa ‘live’.

Totoo ameiambia Saluti5 kuwa anapokuwa na show zikiwemo zile za harusi na sherehe mbali mbali, anakusanya kikosi chake cha kazi na kuliamsha dude.

Kwasasa Totoo anajiandaa kuaichia wimbo wake mpya utakayojulikana kama “Pandisha Kipaja”.

Ndani ya wimbo huo, Totoo ametesa na rap zake kali kupitia mapigo ya kiafrika (afro beat) yanayofanya kibao hicho kichezeshe kuanzia sekunde ya kwanza hadi ya mwisho.

Katika “Pandisha Kipaja”, kuna sehemu Totoo anasema yeye hajaja kuimba bali amekuja kuchezesha. Na kwa hakika wimbo huo utawachezesha watu ile mbaya labda fitna tu zimwangushe.


No comments