TOTTENHAM HOTSPUR YAIKALISHA CRYSTAL PALACE


Heung-Min Son ameifungia Tottenham Hotspur bao pekee dhidi Crystal Palace katika mchezo mkali wa Ligi Kuu uliochezwa katika uwanja wa Wembley.

Nyota huyo wa kimataifa wa Korea Kusini mwenye umri wa miaka 25, alifunga bao hilo katika dakika ya 64 baada ya piga nikupige kwenye lango la Crystal Palace.


Dakika ya 57 winga  Wilfried Zaha wa Crystal Palace alishindwa kutumia nafasi ya dhabu pale alipobaki yeye na kipa Paulo Gazzaniga na kufanikiwa kumlamba chenga kabla hajapiga shuti lililokwenda nje.

No comments