Habari

TWANGA PEPETA YAENDELEZA MAKAMUZI BULYAGA TEMEKE

on

TWANGA Pepeta Sugu “Kisima cha
Burudani” kama kawaida yao jana Ijumaa walifanya makamuzi ndani ya Bulyaga
Temeke na kukonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliohudhuria.
Waimbaji Luiza Mbutu, Haji BSS,
Kalala Junior, Dogo Joshua, J4 Sukari pamoja na marapa Msafiri Diof na Mirinda
Nyeusi walikuwa kivutio tosha, hasa pale walipokuwa wakinogesha kila wimbo
uliokuwa ukirindimishwa.

Kadhalika, wanenguaji Super
Nyamwela na Maria Salome nao walichangia kuifanya shoo ya jana kuwa ni iliyojaa
msisimko wa aina yake kwa wapenzi wao. Pata picha 15 za namna mambo
yalivyokwenda jukwaani.
 Gitaa la Kati “Rythm” likiungurumishwa vilivyo na God Kanuti
 Mwimbaji chipukizi Dogo Joshua akiimba kwa hisia kali
 Mnenguaji Super Nyamwela akiwa kazini
 Hapa J4 Sukari akifukia mashimo 
 Mkaanga Chips James Kibosho akifanya yake jukwaani na kuwatia mzuka zaidi mashabiki
 Mwimbaji Kalala Junior akiwakoleza wapenzi wao
 Maria Salome hakuwa nyuma katika kuhakikisha anawachengua mashabiki wao
 Hapa Kalala Junior na Luiza Mbutu wakiimba kwa pamoja na kuwa kivutio kikubwa
 Mpapasa kinanda Victor Mkambi akiwajibika
 Rapa Msafiri Diof akichengua na rapa zake kali
 Gitaa la Besi la Jojo Jumanne likisisimua
 Charlz Baba akiimba kibao maarufu “Mwana Dar es Salaam”
 Luiza akitoa raha kwa sauti yake tamu ya kumkurupusha nyoka pangoni
 Miraji Shakashia akichana nyuzi za gitaa la Solo
Rapa Mirinda Nyeusi akifukia mashimo

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *