UZINDUZI WA RIVER MUSIC BAND SASA NI BAADA YA MVUA


RIVER Music Band bado inajipanga kwa ajili ya kutoa tarehe nyingine ya uzinduzi baada ya uzinduzi wao uliokuwa ufanyike Jumamosi iliyopita kutibuliwa na mvua kubwa iliyokung’uta siku hiyo.

Kiongozi wa River Music band, Chacha Tumba ameiambia Saluti5 muda mfupi uliopita kuwa wanachosubiri kwa sasa ni kukatika kwa mvua ambazo bado zinaendelea, ili kupanda upya tarehe nyingine ya uzinduzi.

“Mara tu baada ya mvua hizi kukatika tutatangaza tarehe nyingine ya uzinduzi wa bendi yetu na kuwaalika wadau pamoja na mashabiki,” amesema Chacha Tumba.

River Music Band ambayo maskani yake makuu yapo Kibaha Picha ya Ndege mkoani Pwani, inakusanya nguli wengi wa miondoko ya dansi waliowahi kufunika katika bendi nyingine mbalimbali huko nyuma.  

No comments