WAC CASABLANCA WAIBWAGA AL AHLY YA MISRI 1-0 NA KUTWAA TAJI LA KLABU BINGWA AFRIKA


WAC Casablanca ya Morocco ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani, imeichapa Al Ahly ya Misri 1-0 na kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League).

Katika mchezo wa kwanza wa fainali uliochezwa Misri wiki iliyopita, timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Bao lililopeleka kilio kwa miamba ya Misri lilikuja kunako dakika ya 70 pale Ben Charqi alipoambaa wingi ya kulia na kumwacha El-Sulaya kabla hajamimina krosi iliyomaliziwa kwa kichwa na Walid El-Karti.


Mara ya mwisho WAC Casablanca ilitwaa kombe hili mwaka 1992.

No comments