WAZEE WA NGWASUMA KAMA MEEDA CLUB LEO… kesho New Kilimani, Jumapili Coco Beach


BENDI ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma” inayoongozwa na rais Patcho Mwamba leo inatarajiwa kumimina burudani ndani ya Meeda Club, Sinza, jijini Dar es Salaam kama ilivyo kawaida kwa siku za Ijumaa.

Kesho Jumamosi wababe hao wa muziki wa dansi wataunguruma New Kilimani, Kimara Temboni, kabla ya Jumapili kumalizia uhondo wa wikiendi pale Coco Beach kwenye bonanza la kistaarabu kuanzia majira ya saa 10:00 jioni hadi saa 6:00 usiku.

“Tunawaomba mashabiki wote kuhudhuria kwa wingi wakiwa na familia zao (kwa siku za Jumapili), ili kupata burudani kutoka Ngwasuma wabishi wa dansi la kisasa,” imesema sehemu ya taarifa ya bendi hiyo.

No comments