WYCLEF JEAN AWATAKA VIJANA WA URENO KUTOKATA TAMAA KATIKA MAFANIKIO

MSHINDI mara tatu wa tuzo za Grammy, Wyclef Jean amewataka vijana wa Ureno kutokata tamaa ikiwa wanataka kupiga hatua katika jambo lolote wanalofanya kwa sababu maisha ni safari ndefu.

Jean hapo kabla alikuwa akiimba HipHop kwenye kundi la Fugees lakini baadae akabadilisha staili ya kazi na kuanza kupata soko kiasi cha kufanya kazi na mastaa wakubwa akiwemo Shakira.

“Unahitaji kuwa mvumilivu na mwenye hali ya kupambana usikatishwe tamaa na yeyote anasema huwezi kufanikiwa kwa kile unachokiendea,” alisema staa huyo alipokuwa Ureno.

Jean amesema kuwa baada ya kuhamia Marekani akitokea Haiti alilazimika kufanya kila shughuli iliyopo mbele yake ili kutafuta njia ya kufanikiwa kwenye muziki.

“Wakati mwingine unaweza kudhani upo chini lakini kumbe wapo watu ambao wapo chini kuliko wewe, huhitaji kukata tamaan kwa lolote."


“Nilihisi mafanikio nilipopata fursa ya kumuandikia wimbo wa "My Love is Your Love" staa mkubwa Whitney Houston."

No comments