YANGA MIKONONI KWA HANS PLIUJIM JUMAMOSI HII ...Kamusoko, Juma Abdul, Ngoma na Tambwe pigo Jangwani


MECHI ya Yanga na Singida United inatarajiwa kuchezwa Jumamosi hii katika uwanja wa Namfua, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu kwa Pliujim kukutana na timu yake ya zamani.

Miongoni mwa wachezaji nyota wa Yanga ambao hawajasafiri na timu hiyo ni pamoja na kiungo Thaban Kamusoko, Juma Abdul na washambuliaji Donald Ngoma na Mrundi Amissi Tambwe.

Kamusoko, Ngoma na Tambwe ni majeruhi wakati Juma Abdul hakwenda kwa sababu ya kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Timu ya Yanga itacheza na Singida United ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya mtani wake, Simba SC katika mchezo uliopigwa Jumamosi iliyopita uwanja wa Uhuru.

Mpaka wakati huu klabu ya Yanga imejikusanyia jumla ya pointi 16, ikiwa inalingana na timu za Azam FC, Mtibwa Sugar na Simba.

No comments