ZLATAN IBRAHIMOVIC NA PAUL POGBA WAKO FITI KUIVAA NEWCASTLE


Hatimaye Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wamepona na wataorodheshwa katika kikosi cha Manchester United kitakachovaana na Newcastle kwenye mchezo wa Premier League utakaochezwa Old Trafford Jumamosi hii.

Mshambuliaji Ibrahimovic , 36, bado hajashirikishwa katika mechi yoyote msimu huu tangu apate jeraha la goti mnamo mwezi Aprili, lakini baada ya kushiriki mazoezi kwa siku tatu, anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji wa akiba kwenye mchezo huo dhidi ya Newcastle.


Kiungo wa kati Paul Pogba , 24, hajaichezea timu yake tangu alipopata jeraha la nyuma ya goti dhidi ya klabu ya Basel mnamo mwezi Septemba.

No comments