AL JAZEERA WASOGEZA MBELE SHOO YAO YA "FUNGA MWAKA" TANGA... sasa ni Januari Mosi badala ya siku ya mkesha

BENDI ya mipasho ya Al Jazeera imewaomba radhi mashabiki wake wa jijini Tanga kufuatia mabadiliko ya shoo yao maalum ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2018 ambayo ilikuwa ifanyike kesho Jumapili, Desemba 31 ndani ya Splendid Hall.

Shoo hiyo sasa imepangwa kuunguruma Jumatatu, Januari Mosi hivyo wapenzi na wadau wameombwa kujitokeza kwa wingi ili kufurahia mwaka mpya wakiwa na bendi yao inayotikisa vilivyo hapa nchini, hususan katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam.

Kiingilio katika shoo hiyo itakayoanza majira ya saa 3:00 usiku na kuendelea hadi majogoo, kitakuwa sh. 4,000 tu ambapo vibao mbalimbali vya “old is gold” vitaungurumishwa.

No comments