ARSENAL YAIFYATUA CRYSTAL PALACE …Sanchez noma, pasi ya Wilshere yaleta raha


Arsenal imetakata kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Crystal Palace 3-2.

Ikicheza ugenini kwenye dimba la Selhurst Park, Arsenal ikafanikiwa kwenda mapumziko ikiwa mbele 1-0 kwa bao la beki Shkodran Mustafi lililotinga wavuni dakika ya 25.

Dakika ya 49 Andros Townsend akaisawazishia Crystal Palace baada ya kuunganisha vizuri pasi ya winga Wilfried Zaha.

Alexis Sanchez akaipatia Arsenal bao la pili dakika ya 62 kabla ya kufunga goli la tatu dakika ya 66.

Bao la tatu la Arsenal ndilo lililozua gumzo zaidi kufuatia pasi ya ‘maajabu’ ya kiungo Jack Wilshere ambaye alipiga pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja na kutua moja kwa moja kwa Sanchez aliyekuwa kwenye mstari wa 18 ya Crystal Palace na kumtungua kirahisi kipa Julian Speroni.

Crystal Palace wakapunguza aibu kwa kufunga goli la pili dakika ya 87 mfungaji akiwa ni James Tomkins.
No comments