ASANTE KWASI NUSU LIPULI FC NUSU SIMBA SC

MFUMO wa usajili wa Shilikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa njia ya mtandao, maarufu kama "TMS" umefunguliwa tena kwa ajili ya Ligi Kuu na daraja la kwanza Tanzania Bara. 

Desemba 15, mwaka huu mfumo wa usajili kwa njia ya TMS ulifeli, hali iliyosababisha klabu kushindwa kukamilisha usajili kwa wakati kwa mfumo huo.

Pamoja na kufanikiwa kumpa mkataba  dakika za mwisho, lakini Simba ilikuwa kwenye hatihati ya kumtumia Asante Kwasi kwenye michuano ya Ligi hiyo baada ya jina lake kutoonekana kwenye mitandao na kuonesha kuwa bado  hajakamilisha.

Klabu ya Simba ilikuwa haina uhakika wa kaumtumia beki Asante ambae imemsajili kwenye dirisha dogo, ingawa kiasi cha fedha kimefichwa.

Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kwamba mtandao huo sasa upo wazi.

“TFF inazitaka timu zote sasa kukamilisha husajili kuanzia pale walipokwama. Timu zinatakiwa kisajili kabla ya Desemba 23 mwaka huu,” amesema Lucas.

Aidha kuhusiana na suala la usajili wa Kwasi, Lucas amesema kwamba, Simba wataweza kumtumia mchezaji huyo ma ratu atakapokamilisha usajili wake kabla ya Desemba 23 mwaka huu.


“Simba walifanya usajili wa Kwasi dakika za mwisho kwa hiyo nyakati zile mfumo ulikuwa umezidiwa na baadhi ya nyaraka hazikufika, hivyo kwa kuwa FIFA wenyewe wameufunga na kuongeza siku ili jina hilo lijitokeze ndipo mchezaji huyo ataruhusiwa kuichezea  Simba,” alisema Lucas.

No comments