ASIA UTAMU AFUNGUKA SABABU YA KUTOSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA

MWANAMIPASHO Asia Utamu ameweka wazi kuwa hana posti kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na tukio la siku yake ya kuzaliwa kutokana na ukweli wa simanzi na majonzi uliojificha kwenye siku hiyo.

Asia amesema kuwa kwa upande wake ni siku iliyotengeneza historia ambayo inabaki kuwa kumbukumbu katika muda wake wote atakaoishi ulimwenguni ambapo amesema kuwa amepanga kufunguka zaidi mwezi Januari, mwaka ujao.

“Jina langu la pili naitwa FARAJA, ili mjue kwanini sisherehekei tukio la kuzaliwa kwa tarehe husika ntawajuza rasmi Januari tarehe za mwanzo ndo nimepanga kusherehekea, nasikitika sana ni siku ya kuzaliwa lakini ina siri nzito mpaka nimebakia mpweke,” amesema Asia.


“Ewe Mola wangu mpe mama yangu kitabu chake kwa mkono wa kulia, jaman machungu yakipita tukiwa hai mtakula keki msiwazee,” ameongeza mwimbaji huyo aliyepata kutamba na kibao cha “Sioni Thamani ya Pendo”.

No comments