AUDIO: FUNGA MWAKA NA KITU "TUFURAHI NA MWAKA MPYA" CHA BANTU GROUP
TUKIWA tumebakisha masaa machache kuingia mwaka mpya wa 2018, si vibaya ukaburudika na kibao kinachosherehesha shamrashamra za mwaka mpya kutoka Bantu Group, bendi iliyokuwa chini ya mkongwe wa gitaa la Solo, Komandoo hamza Kalala.

“Tufurahi na Mwaka Mpya” ambacho ni makucha yake mwenyewe Komandoo Kalala, kimerekodiwa mwaka 1993 katika Studio za RTD, huku washiriki wake wakiwa ni pamoja na waimbaji; Ally Choky, Mwinjuma Muumin, Musemba wa Minyugu na mwenyewe Kalala aliyeimba na kupiga Solo.

Gitaa la Rythym katika wimbo huu ni kazi ya Mangele Sange, Rashid Kalala (Bass) na Ally Adinan (Second Solo), Michael Liloko (Drums) na Alama Shomvi (Tumba).

Sauti wa ndege wa porini anayefurahia kumaliza mwaka ndio inayoanzisha wimbo huu ambapo hata hivyo sauti hiyo si ya ndege halisi bali ni mnenguaji wa bendi hiyo Mapunda (marehemu kwa sasa) aliyeamua kunogesha.  

No comments