BANANA ZORRO ATIMIZA MIAKA KUMI YA NDOA YAKE... atoa neno zito kwa "machalii" wenzie

BOSI wa B Band, Banana Zorro leo ametimiza miaka kumi ya ndoa yake ambapo ameposti kwenye mitandao ya kijamii picha aliyopiga na mkewe hukua akiachia ujumbe mzito kwa vijana wa sasa.

Katika posti hiyo, kwanza Banana amemuhakikishia mke wake kwamba anampenda sana wakati huu wakiwa wanafurahia muongo mmoja tangu waoane, huku akimweleza kuwa anampenda sana.

Kisha, akamalizia na meseji kali kwa vijana wenzie akiwaambia kwamba kudumu kwa muda mrefu kwenye ndoa inawezekana iwapo tu utamwamini Mungu na kumuweka mbele.

“Happy 10th anniversary bebe......Nakupenda Sana....Allah azidi kutujaalia.....#kijana inawezekana ndoa yako ikadumu ukimtanguliza Mungu....” ameandika Banana kwenye posti hiyo.

No comments