BEYONCE KULIAMSHA "DUDE" HARUSI YA GARETH BALE

IMERIPOTIWA kuwa Mrembo Beyonce atakuwa mtumbuizaji kwenye harusi ya staa wa timu ya Real Madrid Gareth Bale raia wa Wales.

Bale anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake Emma Rhs-Jones ambaye amezaa nae watoto wawili gazeti la The Sun limeripotiwa kuwa mazungumzo bado yanaendelea lakini huku Beyonce akidaiwa kuwa anahitaji Dola Milioni 1.5 kama sehemu ya malipo yake.

Gareth Bale na mke wake hivi sasa wanaishi Hispania lakini wamepanga kufungia ndoa nchini Italia.

Staa huyo mwenye mkataba na timu ya Real Madrid amekuwa akilipwa pauni 300,000 kwa wiki.


Beyonce amekuwa akitoa burudani za sherehe za harusi kwa dau La Dola milioni 3.9.

No comments