BOSI WA SINZA SOUND BAND ASHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA KWENYE KITUO CHA WATOTO YATIMA

BOSI wa Sinza Sound Band, Said Kaunga amebainisha kuwa hakuna jambo lililompa furaha kwenye maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ya mwaka huu kama lile tukio la kula keki ya “birthday” pamoja na watoto yatima.


Kaunga amesema kuwa amefurahi kuona watoto hao aliowatembelea ghafla kituoni kwao wamefarijika kwa kuona kwamba na wao wanakumbukwa na jamii, ambapo ametoa wito kwa watu wengine wa madaraja mbalimbali kujitokeza kuiga kile alichokifanya yeye. 

No comments