CHELSEA HATARINI KUPANGIWA PSG AU BARCELONA …Atletico bye bye Champions League, Barcelona, Juventus moto chini


Chelsea imetoka sare ya 1-1 na Atletico Madrid kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa kundi C, matokeo yanayoitupa nje miamba hiyo ya Hispania.

Chelsea inamaliza hatua ya makundi kwa kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi 11 sawa na Roma ya Italia iliyokaa kileleni kwa faida ya wastani wa magoli.

Atletico ilipata bao la kuongoza dakika ya 56 mfungaji akiwa ni Saul Niguez lakini goli la kujifunga la Stefan Savic dakika ya 76, likaipatia pointi moja Chelsea.

Kuna uwezekano mkubwa sana wa Chelsea kukutana na Paris Saint-Germain, Barcelona au Besiktas kwenye hatua ya mtoano ya 16 bora.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JUMANNE:
Kundi A:
Benfica 0 - 2 Basel
Manchester United 2 - 1 CSKA Moscow
Zilizopenya 16 bora ni Manchester United na Basel
Kundi B:
Bayern Munich 3 - 1 Paris Saint Germain
Celtic 0 - 1 Anderlecht
Zilizopenya 16 bora ni PSG na Bayern Munich
Kundi C:
 Chelsea 1 - 1 Atletico Madrid
Roma 1 - 0 Qarabag FK
Zilizopenya 16 bora Roma na Chelsea
Kundi D:
Barcelona 2 - 0 Sporting CP
Olympiacos 0 - 2 Juventus
Zilizopenya 16 bora ni Barcelona na Juventus

No comments