CHRIS BROWN MSHIKEMSHIKE NA DEMU MPYA WA KIINDONESIA

PICHA aliyoposti rapa Chris Brown akiwa studio na mrembo matata imeanza kuibua hisia kuwa huenda ni mpenzi wake mpya.

Rapa huyo hajawahi kutulia kwenye uhusiano wa kimapenzi tangu apigwe chini na mrembo Rihanna kisha akaja kutemwa tena na Karrueche Tran.

Picha aliyotuma Brown kwenye mtandao wa Instagram inamuonyesha akiwa na Agnez Mo ambaye ni mwimbaji kutoka Indonesia.

Mo ni mwanamuziki tajiri nchini Indonesia akiwa anaongoza kwa mauzo ya nakala zake kwa miaka mingi mfululizo.


Mwimbaji huyo ni mzaliwa wa Jakarta, yupo nchini Marekani kwa masuala ya kimuziki ambapo anataka kukamilisha albamu yake.

No comments