DONALD NGOMA SASA AINGIZWA MTEGONI

KITENDO Cha mshambuliaji wa timu ya Yanga Donald Ngoma kujumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 29 walioitwa kujiunga na kambi ya Timu ya Taifa ya Zimbabwe kwa ajili ya michuano ya kombe la Chalenje nchini Kenya mwezi ujao kimemuwashia taa Nyekundu staa huyo.

Ngoma anaripotiwa kuondoka klabuni bila taarifa kwenda nchini huku uongozi wa timu hiyo angerejea nchini Tanzania wakati wowote lakini mpaka sasa imekuwa kimya.

Yanga inatambua kuwa Ngoma ni mgonjwa na kama yupo fiti kiasi cha kuitwa timu ya taifa ina maana alikuwa akifanya ujeuri.

Taarifa zilizofika kwenye gazeti hili ni kuwa mshambuliaji huyo kuna uwezekano mdogo kuendelea kuitumikia Yanga baada ya kujipalia moto mwenyewe.

Licha kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Ngoma hakuwa na mwanzo mzuri kwani amefanikiwa kufunga bao moja tu mpaka sasa kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo imesimama kupisha mechi za kimataifa.

Michuano ya Kombe la Chalenji kwa mwaka huu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Desemba 3 na kufikia ukomo Desemba 19 ikishirikisha timu kumi.

Zimbabwe imepangwa Kundi B ikiwa na timu za Uganda ambao ndio mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Sudan Kusini, Ethiopia na Burundi.

Kikosi kizima cha Zimbabwe kinahusisha makipa Elvis Chipezeze, Herbert Rusawo na Takabva Mawaya.

Walinzi: Divine Lunga, Praise Tonha, Qadr Amini, Partson Jaure, Farai Madhananga, Peter Muduhwa, Jimmy Dzingai, Collin Kwaramba, Kelvin Moyo na Steven Makatuka.

Viungo ni Devon Chafa, Gerald Takwara, Never Tigere, Liberty Chakoroma, Rodwell Chinyengetere, Ishmael Wadi, Raphael Manuvire, Ali Sadiki, Clemence Matawu na Martin Vengesai.


Washambuliaji ni pamoja na Dominic Chungwa, CliveAugusto, Terrence Dzukamanja, Donald Ngoma na Lot Chiwunga.

No comments