DORTMUND YAANZA KUMNYATIA HENRIKH MKHITARYAN

KLABU ya Borussia Dortmund imeanza kumnyemelea kiungo wa timu ya Manchester United, Henrikh Mkhitaryan.

Kiungo huyo mwenye miaka 28 hana maelewano na kocha wake Jose Mourinho kwa sababu ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza.


Hata hivyo, Borussia inaweza kukumbana na upimzani kutoka Arsenal ambao wamepanga kumaliza dili hilo mwezi Januari.

No comments