EMINEM AKIRI DR DRE AMECHANGIA MAFANIKIO YAKE

RAPA mtukutu ambaye anahusudu watu weusi duniani, Eminem amesema kuwa uwepo wa Dr. Dre umechangia kiasi kikubwa cha mafanikio ya kazi zake.

Eminem amesema kwamba Dr Dre mbali na masuala ya kazi za muziki lakini pia ni mshauri na mlezi bora wa vijana.

“Nimekua na Dre kwa miaka mingi na sikuwahi kuona mapungufu yake, ni kiongozi na mshauri mzuri kwa vijana,” alisema Eminem.

“Ukiachilia mbali usimamizi wake kwa kazi zangu Dr amekuwa mshauri wangu mzuri, mafanikio yangu yana mkono wake,” aliongeza.


Studio ya Dr Dre ndio inahusika moja kwa moja na uzalishaji wa nyimbo za Eminem, rapa anayetajwa kuwa mtata zaidi nchini Marekani.

No comments