FATHER MAUJI AIKUMBUKA JAHAZI MODERN TAARAB

KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni kama baadhi ya waliokuwa wasanii Jahazi Modern Taarab wameanza kuimiss bendi yao hiyo, mcharazaji mahiri wa gitaa la Solo, Mohammed Mauji “Father Mauji” ameposti maneno mazito kwenye ukurasa wake wa facebook akikumbuka wakati walipokuwa kwenye ubora wao.

Katika posti hiyo iliyoambatana na picha ya jukwaani ambayo Father Mauji amepiga na Prince Amigo na aliyekuwa mmoja wa mabaunsa wa bendi hiyo, Hassan Ndevu, mkali huyo wa masebene ameandika:

“Dah enzi hizo Jahazi Modern Taarab imetimia kazi kazi, dairekta mwenyewe Father Mauji, safu ya waimbaj wa kike Khadija Yusuph, Malkia Leyla Rashid Fatma Mcharuko, Fatma Shobo, Mwansit Robert, Miriam Amour, Rahma Machupa, Mwasiti Kitoronto, Fatma Khasim, Mishi Zele, waimbaji wa kiume ikiongozwa na mwenyewe nguli nadhani  mnamjua jina nalihifadhi akifatiwa na Prince Amigo huku Mohamed Ally Mtoto Pori.”


No comments