GOD KANUTI WA TWANGA SASA NI MALI YA TOT BAND …wasanii wengine wawili wa Twanga nao waomba kazi TOT


Mcharaza gitaa la solo wa Twanga Pepeta, God Kanuti sasa ni mali ya TOT Band na wikiendi hii ataandamana na kundi hilo la chama tawala hadi mjini Dodoma.

TOT  itafanya onyesho ndani ya Club La Aziz mjini Dodoma Jumamosi hii kwa kushirikiana na Vijana Jazz Band ambapo Kanuti atakuwa mmoja wa wasanii watakaopeperusha bendera ya TOT.

Mkuu wa Mipango wa TOT, Juma Jerry “JJ Mzee wa Mbezi” ameithibitishia Saluti5 kuwa Kanuti tayari ameajiriwa TOT na kwamba iwapo ataonekana kwenye majukwaa ya Twanga basi itakuwa ni ndondo au kusalimiana kisanii.

“Kanuti ni msanii wetu na tunakwenda nae Dodoma wikiendi hii, alisema JJ na kuongeza kuwa kuna wasanii wengine wawili Twanga wanaomba kazi TOT.

“Yupo mpiga gitaa mmoja na mwimbaji mmoja, hawa nao wanaomba ajira TOT ila bado tunawatathmini kwa kina,” aliongeza JJ.


No comments