HAJI MWINYI: NINA IMANI NA ZANZIBAR HEROES CHALLENGE CUP MSIMU HUU

BEKI wa timu ya taifa ya Zanzibar, Mwinyi Haji amesema kuwa uteuzi wa kocha Hemed Morocco unawafanya wapate imani ya kuibuka mabingwa wa michuano ya Kombe la Chalenji.

Mwinyi amesema kuwa kikosi chao kimejaza wachezaji wengi vijana wenye uchu wa mafanikio, hivyo kuna kila dalili ya kurejesha heshima kupitia michuano hii itakayoanza kutimua vumbi Desemba 3 nchini Kenya.

Zanzibar Heroes imeanza kambi siku nyingi visiwani Zanzibar huku ikicheza michezo mbalimbali ya kirafiki ili kujiandaa na michuano hiyo.

Timu hiyo imepangwa kundi moja na timu za Kilimanjaro Stars, Rwanda, Kenya na Libya.


“Lazima niwe muwazi, nilianza kuvutiwa na kocha siku alipotangaza kikosi chetu kilichosheheni vijana wengi wanaosaka mafanikio, naamini tutafanya vyema kutokana na mseto wa wachezaji uliopo sasa,” alisema Mwinyi.

No comments