HANS PLUIJIM AZOA WANNE SERENGETI BOYS

KOCHA wa timu ya Singida United, Hans Pluijim ni kama amefanya kufuru ya kutaka kubadilisha kikosi kizima baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji sita wapya ili kumuongezea spidi ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu bara.

Pluijim kwa mkupuo amewadaka wachezaji wanne vijana kutoka Serengeti Boys ambao ni Mohammed Abdallah, Ally Hamis, Ng’azi Assad, Ally Juma na Issa Makamba huku kila mmoja akimsainisha mkataba wa miaka mitatu.

Mastaa wengine ni pamoja na Daniel Lyanga ambaye alikuwa na kikosi cha Tanzania Bara kwenye mashindano ya CECAFA Challenge Cup na “Pappy Kambale” raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mastaa hao wawili amewasainisha kwa mkataba wa miaka miwili kila mmoja.


Pluijim amekuwa na mwenendo mzuri katika kikosi hicho ambacho kina safu imara ya ulinzi lakini amekuwa akilaumiwa kwa kuwa na washambuliaji wasiozalisha mabao ya kutosha.

No comments