HUSSEIN JUMBE AANIKA SIRI YA WIMBO WAKE “SIRI” KUTUMIWA NA NA RAYVANNY WA WCB


Baada ya Msondo Ngoma kuwasilisha malalamiko juu ya kionjo cha wimbo wao wa “Ajali” kutumiwa na lebo ya WCB kupitia wimbo “Zilipendwa”, WCB wanaingia tena kwenye gumzo la kuchukua hazina nyingine ya muziki wa dansi.

Safari hii ni kupitia msanii wao Rayvanny ambaye wiki hii ameachia kigongo kipya “Siri” aliomshirikisha Nikk wa Pili.

Katika wimbo huu “Siri”, Rayvanny amerudia kwa sehemu kubwa wimbo wa mkongwe Hussein Jumbe “Siri ya Nini”.

Wakati mashabiki wengi wakijiuliza juu ya uhalali wa Rayvanny kutumia kazi hiyo, Hussein Jumbe mwenyewe anaitaarifu Saluti5 kuwa alitoa Baraka zote kwa msanii huyo wa WCB.

“Rayvanny alinifuata kuhitaji kutumia sehemu ya wimbo wangu, sikuwa na hiyana, nilimruhusu na nashukuru pia alinipatia kifuta jasho,” anaeleza Hussein Jumbe.

“Hata katika video ya wimbo huo mwishoni kabisa utaona uwepo wangu, hiyo ni kudhihirisha kuwa nilishirikishwa katika hatua zote,” anafafanua Hussein Jumbe.

No comments