INEM PETER AANIKA SIFA ZA MWANAUME ANAYETAKA AOLEWE NAE

STAA wa filamu asiyeishiwa vituko kwenye mitandao ya kijamii, Inem Peter ametoa tena kituko kingine baada ya kuanika sifa za mwanaume anaetaka kumuoa.

Inem amesema kuwa anahitaji mwanaume mwenye fedha ya kutosha na awe mrefu kumzidi yeye.

“Kwa sasa sina mpenzi lakini nahitaji mtu tajiri na mrefu aweze kunioa, hizo ndio hisia zangu,” ilisomeka sehemu ya taarifa fupi aliyotuma.

Staa huyo ambaye anasifika kwa uandishi bora wa miongozo ya filamu alisema anavutiwa na watu wenye mionekano kama John Dumelo, Wole Ojo, Jibola Dabo, Mike Godson na Frederick Leonard.


“Nina urefu wa futi tano, nahitaji mwanaume mrefu kunizidi mimi lakini lazima awe na fedha ya kutosha.

No comments