ISHA MASHAUZI AINGIA STUDIO KUPAKUA KITU KIPYA CHA MIONDOKO YA ZOUK


Baada ya ngoma zake tatu za miondoko ya rumba na afro beat kufanya vizuri sana, hatimaye Isha Mashauzi ameingia studio kuandaa kigongo kipya cha miondoko ya zouk.

Isha ambaye anashikilia tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa taarab, amedhihirisha kuwa yeye ni staa hadi nje ya taarab kupitia nyimbo “Nimlaumu Nani”, “Nimpe Nani” na “Jiamini” ambazo zimefanya vizuri sana katika miaka ya hivi karibuni.

Wiki iliyopita, Isha Mashauzi akaingia studio za Soft Records chini ya producer Pitchou Mechant kwaajili ya kupika wimbo utakaokwenda kwa jina la “Stress” ambao umepigwa katika miondoko ya zouk na kuchanganywa na vionjo vingine vya muziki wa kiafrika (Afro Beat).

Isha ameiambia Saluti5 kuwa wimbo “Stress” utatoka mwezi Machi, lakini mwezi Januari ataachia wimbo “Nibembeleze” ambao upo katika miondoko ya afro beat.

“Kwasasa nimeamua kuwa kila baada ya miezi miwili nitakuwa nikiachia ngoma mpya katika audio na video, nina akiba ya nyimbo nyingi sana,” alisema Isha na kuwataka mashabiki wake wakae tayari kwa audio na video ya “Nibembeleze”.
 Isha Mashauzi ndani ya studio za Soft Records
 Isha Mashauzi akisikiliza kazi yake mpya
 Isha akielekeza jambo kwa producer Pitchou Mechant
 Kazi mpya ya Isha ikiwa jikoni
Hosea Bass akipiga gitaa la bass katika wimbo mpya wa Isha Mashauzi

No comments