JELA YAMNUKIA NYOSH EL SAADAT

KUNA tetesi kuwa rais wa vijana, Nyosh el Saadat anampigisha kazi kijana Ally Said “Kelly Haso” kwenye kundi lake jipya la muziki huku ikiwa kijana huyo ana mkataba na kampuni ya Nyegera waitu Entertainment.  

Uongozi wa kampuni ya Nyegera Waitu umechonga na Saluti5 na kubainisha kuwa wamenyetishiwa kwamba Kelly Haso amejiunga kinyemela na kundi jipya la muziki lililo chini ya Nyosh El Saadat hivyo wamepanga kuchukua hatua kali za kisheria.

“Tutakachokifanya ni kumpeleka Nyosh mahakamani kwani tuna nyaraka zote za mkataba tuliofunga na msanii Kelly, kwahiyo tutadai fidia kutokana na kumvunjisha mkataba,” amesema mnene wa Nyegera Waitu, tabibu Ntamba na Mungu.

Kwa mujibu wa Ntamba na Mungu, Kelly aliingia kwenye kampuni yake kama mwanafunzi na alikuwa bado anachuliwa kwa nmakubaliano maalum huku akiwa tayari kesharekodi kichupa cha “Natamani” chini ya kampuni yake.


Saluti5 inamtafuta Nyosh El Saadat ili kupata kauli yake kuhusiana na sakata hilo na tunawaahidi kukimwaga bayana kile atakachosema mara tu tutakapozungumza nae.

No comments