JENNIFER LOPEZ, MARC ANTONY FULL BATA KWA RAHA ZAO

MREMBO Jennifer Lopez na staa Marc Antony wamesahau tofauti zao kwa muda na kuamua kujiachia pamoja wakila bata ili kufariji watoto wao mapacha.

Wawili hao waliachana mwaka 2011 baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 7 na kila mmoja kuamua kusaka mpenzi mpya lakini hivi karibuni wamenaswa pamoja wakiwa sambamba na watoto wao mapacha.

“Hatuna ugomvi wowote, tunaendelea kushirikiana kwasababu watoto wanatuunganisha, ni vyema wakati mwingine kujumuika pamoja kwa muda mfupi,” ilisomeka sehemu ya taarifa fupi aliyotuma Jennifer kwenye mitandao ya kijamii.


Jennifer hivi sasa anaishi na mpenzi mpya kijana Alex Rodriguez ambaye amekuwa akizuunguka nae kila sehemu anayokwenda.

No comments