JKT RUVU YAINGIA KAMBINI IKIPANIA KUREJEA LIGI KUU

TIMU ya JKT Ruvu imeingia kambini kuanza maandalizi ya mzunguuko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania bara, ikiwa chini ya kocha wake, Bakari Shime.

Msemaji wa JKT Ruvu, Constantine Masanja amesema kuwa wachezaji wote wameingia kambini kwa wakati na hakuna matatizo binafsi wala majeruhi.

“Timu iko kambini na wachezaji wote wamerejea kambini na hatuna mchezaji aliyewasilisha matatizo binafsi wala hakuna majeruhi,” amesema.


Aidha, Masanja amesema kuwa JKT Ruvu imejipanga vizuri katika michezo iliyosalia na lengo la timu ni kurejea Ligi Kuu msimu ujao.

No comments