Habari

JOSE MOURINHO AAMBIWA YEYE SI CHOCHOTE MBELE YA PEP GUARDIOLA …ishu sio pesa bali kiwango cha ufundishaji

on

Beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher anaamini sio mambo ya ‘fwedha’ tu ndiyo yanayozitenganisha klabu za Manchester City na Manchester United kimafanikio, bali kuna zaidi ya hilo.
Carragher ambaye ni mchambuzi wa soka, anadai aina ya ufundishaji kati makocha Pep Guardiola na Jose Mourinho, ni sababu kubwa iliyopelekea timu hizo kuachana kwa tofauti ya pointi 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Beki huyo wa zamani wa Liverpool anaamini kama Guardiola angekuwa kocha wa Manchester United, basi ingetwaa ubingwa msimu.
“Kama Mourinho angekuwa anaifundisha Manchester City, basi isingeweza kutandaza soka tunaloliona sasa hivi. Kama kuna mchezaji ‘uti wa mgongo’ wa Manchester City, huyo si mwingine zaidi ya Kevin De Bruyne, mchezaji ambaye Mourinho alimfundisha Chelsea lakini akampiga bei,” anaeleza Carragher.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *