KAGERA SUGAR YASEMA HAITASHUGHULIKA NA USAJILI WA DIRISHA DOGO

KLABU ya Kagera Sugar pamoja na kuwa na mwanendo wa kusuasua katika michuano ya Ligi Kuu Bara, lakini haina mpango wa kuingia sokoni kwa pupa kusaka mastaa wa kuwapiga jeki ili kuepukana na balaa la kushuka daraja.

Kocha mzoefu, Mecky Mexime alisema kuwa haoni sababu matokeo wanayoyapata ni sehemu ya mchezo tu ya timu kupitia kwenye kipindi kigumu.

Kocha huyo alisema kuwa ana imani kikosi chake kitazinduka na kuanza kufanya vyema hivyo dirisha hili halimpasui sana kichwa.

“Sina mpango wa kutema mchezaji yeyote hapa hawa nilionao wanatosha, ni matokeo tu ya kimchezo ni kama upepo mbaya ulitupitia lakini kila kitu kitakwenda sawa,” alisema kocha huyo.

Kikosi cha Kagera Sugar kina changamoto ya kukosa umakini katika umaliziaji huku safu yake ikiwategemea zaidi Venance Ludovick na Edward Christopher “Edo” ambao wamepoteza makali.

No comments