KAMUSOKO UWANJANI JANUARI MWAKANI

HALI ya kuingo wa timu ya Yanga Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko imeanza kutengemaa ambapo ripoti kamili kutoka kwa madaktari inaeleza kuwa staa huyo anaweza kuanza kuingia uwanjani ifikapo Januari mwakani.

Kamusoko anatibiwa na jopo la madaktari wa hospitali ya Temeke ambao wana mapenzi na klabu ya Yanga.

Katibu wa chama cha madaktari wa michezo Tanzania Dk. Nassor Matuzya amesema kwamba vipimo walivyomfanyia Kamusoko vinaonyesha kuna tatizo ndani ya goti lake la mguu wa kushoto ambapo sasa atalazimika kukaa nje kupisha matibabu ya wiki mbili ndipo aruhusiwe kukanyaga uwanjani.

“Niweke wazi tu kuwa Kamusoko atarejea uwanjani Januari akiwa mwenye nguvu zaidi na tatizo hili halitamsumbua tena,” amesema Dk. Matuzya ambaye ameunda jopo la madaktari wenye mapenzi na Yanga katika hospitali ya Temeke kumtibu mchezaji huyo.


Daktari huyo wa zamani wa Yanga alijitolea kuunda jopo la madaktari baada ya kuguswa na maumiwu ya mchezaji huyo ambaye yuko nje kwa muda mrefu na kushindwa kuisaidia timu yake.

No comments